| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Kilipukaji. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Noda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni Ondoa watu wote na uzime moto kutoka mahali inayostahimili mlipuko.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko.
|
Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kujisikia joto na kujaa usoni. Kushuka kwa mapigo ya moyo. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Udhaifu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ishara: E, T+ R: 3-26/27/28-33-52/53 S: (1/2-)33-35-36/37-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 1.1D | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto. Hifadhi kwenye jengo lililotengwa. Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU HATARI KWA MWILI: Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Humenyuka pamoja na asidi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): MAK: IIb (ona Vidokezo); H (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, mfumo mkuu wa neva na damu kusababisha kuharibika kwa utendaji na kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa kusababisha ugonjwa wa moyo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 0.9kPa: 139°C Kiwango myeyuko: 2°C Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.5 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. MAK value not established but full documentation is available (MAK IIb).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||