o-sec-BUTYLPHENOL ICSC: 1472
Oktoba 2002

2-sec-Butylphenol
2-(1-Methylpropyl)phenol
CAS # 89-72-5 C10H14O / C2H5(CH3)CHC6H4OH
RTECS # SJ8920000 Masi ya molekuli: 150.2
UN # 3145
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Dioksidi kaboni, povu, poda.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. kooni na kifuani. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: endapo mwagiko ni mwingi tumia vazi linalokinga kemikali.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Kinachotenganishwa na anhidridi za asidi, kloridi za asidi, besi, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


o-sec-BUTYLPHENOL ICSC: 1472
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI KAHAWIA-MANJANO AU MANGO.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi, anhidridi asidi na kloridi asidi. Hushambulia chuma, shaba na aloi zake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: kama TWA 5 ppm; (ngozi); (ACGIH 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, na ngozi. Mvuke huu inakera njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 224-237°C
Kiwango myeyuko: 14°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.98
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 10
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.2
Kiwango cha kumweka: 107°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.27
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001