| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
|
| Ngozi |
|
Glavu za kinga.
|
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuchanganyikiwa. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Ainisho ya EU Ishara: Xn, N R: 22-43-48/22-50/53 S: (2-)24-37-60-61 Ainisho ya UN | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA NYEUPE HADI KIJIVU YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. Iwapo kavu, huweza kuchajiwa kiumemetuamo kwa kuzinga, upitishaji nyumatiki, umiminaji, nk. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na oksidi za nitrojeni, oksidi za sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia shaba. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama TWA 2 mg/m³; A4; (ACGIH 2002). MAK: 2 mg/m^3; Sh; Aina ya kiwango cha juu: II(8); Aina ya mimba: D; (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa endokrini, ini, mfumo wa neva na thioridi/kikoromeo kusababisha kuharibika kwa utendaji. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 2.3kPa: 117°C Kiwango myeyuko: 71°C Uzito wiani: 1.3 g/cm^3 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.02 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.9 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Mfiduo wa disulfiram waweza kupunguza uimara wa kuhimili kileo, kuathiri mfumo wa moyo na mishipa na mfumo mkuu wa neva kusababisha kupiga moyo kwa nguvu, kushuka kwa mapigo ya moyo, kupumua kwa kasi. Dalili zinaweza kuchelewa. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Antabuse na Rosulfiram ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||