ISOFLURANE ICSC: 1435
Machi 2002

Ether, 1-chloro-2,2,2-trifluoroethyl difluoromethyl
2-Chloro-2-(difluoromethoxy)-1,1,1-trifluoroethane
CAS # 26675-46-7 C3H2ClF5O
RTECS # KN6799000 Masi ya molekuli: 184.5
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kupoteza fahamu. Tazama Vidokezo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Uingizaji hewa. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


ISOFLURANE ICSC: 1435
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho yanayosababisha ulikaji kama vile fosjini kloridi hidrojeni na floridi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK: IIB (2001)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Mvuke huu inakera njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na mfumo wa moyo na mishipa. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 48.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.5
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 32
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.1
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Forane ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA

LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001