| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 44°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 44°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kutapika.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Ainisho ya EU Ishara: Xn, N R: 10-20-36/37/38-51/53 S: (2-)26-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFI-III
Msimbo wa NFPA: H 0; F 2; R 0;
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yakerayo na yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama isoma zilizochanganyika): 25 ppm; (ACGIH 2001) MAK kama isoma zote: 20 ppm; 100 mg/m^3 class II, 1 C (2001) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kusababisha uchomi wa muda mrefu wa mapafu (chronic bronchitis). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na damu. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 169°C Kiwango myeyuko: -44°C Uzito wiani (maji = 1): 0.88 Umumunyifu katika maji: ni dhaifu Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): Kiwango cha kumweka: 44°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 500°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.9-6.4 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.8 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Ona ICSC 1155 1,3,5-Trimethylbenzene (Mesitylene), ICSC 1362 1,2,3-Trimethylbenzene (Hemimellitene), ICSC 1389 Trimethyl benzene (isoma zilizochanganyika). 1,3,5-Trimethilibensini (Mesitylene) ni uchafu kwa majini.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||