ALLYL PROPYL DISULFIDE ICSC: 1422
Oktoba 2001

2-Propenyl propyl disulfide
Onion oil
CAS # 2179-59-1 C6H12S2 / CH2=CHCH2SSCH2CH2CH3
RTECS # JO0350000 Masi ya molekuli: 148.3
UN # 1993
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Povu, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 56°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 56°C, uingizaji hewa.

MFIDUO


Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kifua kufungana. Kichefuchefu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Mchomo. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Inayotoza machozi.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


ALLYL PROPYL DISULFIDE ICSC: 1422
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO ISIYOKOZA CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha oksidi za sulfuri. Humenyuka pamoja na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: kama TWA 2 ppm (ACGIH 2001). TLV: kama STEL 3 ppm (ACGIH 2001). MAK: 2 ppm; 12 mg/m^3 (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 2.1kPa: 66-69°C
Kiwango myeyuko: -15°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 50
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 56°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001