VALERALDEHYDE ICSC: 1417
Machi 2002

n-Pentanal
Amyl aldehyde
Butyl formal
CAS # 110-62-3 C5H10O / CH3(CH2)3CHO
RTECS # YV3600000 Masi ya molekuli: 86.1
UN # 2058
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kuhara. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-I+II Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kilichofungwa vizuri. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


VALERALDEHYDE ICSC: 1417
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kupata joto na kwa kuathiriwa na asidi iso-kikaboni na besi kwa athari ya moto au mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA (ACGIH 2001).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 103°C
Kiwango myeyuko: -91°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.4 wastani
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 3.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.07
Kiwango cha kumweka: 12°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 222°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-7.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.31
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001