METHYL CHLOROACETATE ICSC: 1410
Oktoba 2001

Chloroacetic acid methyl ester
Methyl monochloroacetate
Methyl-alpha-chloroacetate
CAS # 96-34-4 C3H5ClO2
RTECS # Masi ya molekuli: 108.53
UN # 2295
EC # 607-205-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda kavu, mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 57°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 57°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vya plastiki vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ishara: T
R: 10-23/25-37/38-41
S: (1/2-)26-37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GTF1-I Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


METHYL CHLOROACETATE ICSC: 1410
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho babuzi pamoja na kloridi hidrojeni. Humenyuka pamoja na kinakisishaji na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK: 1 ppm 4.5 mg/m^3 H Sh (DFG 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa ngozi, inakera kwa ukali macho na inakera njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 129.5°C
Kiwango myeyuko: -32.1°C
Uzito wiani: 1.2 g/cm^3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 19.8°C: 5.2
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 650
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02
Kiwango cha kumweka: 57°C o.c.
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 7.5-18.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.76 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001