| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na maji.
|
Moto unapotokea katika eneo: dioksidi kaboni, poda. USITUMIE maji.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Maumivu. Wekundu. Mibabuko nzito ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ishara: C R: 14-20/22-29-35 S: (1/2-)26-36/37/39-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S1836;
Msimbo wa NFPA: H 4; F 0; R 2; W
|
Uingizaji hewa kwenye sakafu. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO AU UWEKUNDU, KIFUKACHO CHENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 140°C huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi. Humenyuka vikali ikiwa na maji kusababisha mafusho yenye sumu ya dioksidi sulfuri na kloridi hidrojeni. Humenyuka pamoja na dutu nyingine nyingi kama vile dutu zinazoweza kuwaka, amini, besi na metali, kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm (kiwango cha juu) (ACGIH 2001). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kali kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mapafu kusababisha kuwashwa na kufungana kwa njia za hewa. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 76°C Kiwango myeyuko: -104.5°C Uzito wiani (maji = 1): 1.64 Umumunyifu katika maji: mmenyuko Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 16 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.49 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||