| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo. Kichefuchefu. Kutapika. Tetemeko.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ishara: T R: 23/25-36/37/38 S: (1/2-)23-37/39-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2T
|
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Baridi. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI ILIYOBANWA AU GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI, ISO HARUFU HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile floridi hidrojeni na oksidi za sulfuri. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: kama TWA 5 ppm (ACGIH 2001). TLV: kama STEL 10 ppm (ACGIH 2001). MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege, kutoweza kupumua. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -55.3°C Kiwango myeyuko: -135.8°C Uzito wiani: 3.72 g/l Umumunyifu katika maji: 4-5 ml/100ml Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21.1°C: 1.7 10^3 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.5 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||