| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kutapika.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kuhara. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Ishara: T, N R: 40-48/23-51/53 S: (1/2-)23-36/37-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1669
Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 0;
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, besi kali, na poda ya metali. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na fosjini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kali poda ya metali na aloi za sodimu-potasiamu kusababisha athari ya mlipuko na yenye sumu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): MAK: 5 ppm; 42 mg/m^3; Aina ya kiwango cha juu: II(2); (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kudidimia kwa utendaji. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva kusababisha kuharibika kwa utendaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 162°C Kiwango myeyuko: -29°C Uzito wiani (maji = 1): 1.68 Umumunyifu katika maji: fukara kabisa Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 25°C: 0.453 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.67 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||