PROPYLENE GLYCOL DINITRATE ICSC: 1392
Oktoba 2001

1,2-Propanediol dinitrate
PGDN
CAS # 6423-43-4 C3H6N2O6 / CH3CHONO2CH2ONO2
RTECS # TY6300000 Masi ya molekuli: 166.09
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Kilipukaji. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Isodhurika kwa moto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


PROPYLENE GLYCOL DINITRATE ICSC: 1392
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Inapowaka hutengeneza gesi babuzi na zenye sumu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm; kama TWA (ngozi) (ACGIH 2001) MAK: 0.05 ppm; 0.3 mg/m^3 ngozi (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi au kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 121°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2 ifikapo 25°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.1
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 22.5°C: 9.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.73
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001