CYANOGEN ICSC: 1390
Oktoba 2001

Dicyanogen
Ethanedinitrile
Oxalonitrile
(silinda)
CAS # 460-19-5 C2N2
RTECS # GT1925000 Masi ya molekuli: 52.04
UN # 1026
EC # 608-011-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji vikali.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Degedege. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Ishara: F, T, N
R: 11-23-50/53
S: (1/2-)23-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 2.1

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2TF Msimbo wa NFPA: H 4; F 4; R 2;
Isodhurika kwa moto. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


CYANOGEN ICSC: 1390
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI AU GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa. na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi zenye sumu kama vile sianidi hidrojeni, monoksidi kaboni, oksidi za nitrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii humenyuka pamoja na asidi kusababisha gesi zenye sumu sana kama vile sianidi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm; kama TWA (ACGIH 2001) MAK: 10 ppm; 22 mg/m^3 (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kutoweza kupumua na kuanguka kwa udhaifu. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -21.2°C
Kiwango myeyuko: -27.9°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.95 ifikapo -21°C
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 450
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.8
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 6.6-42.6
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.07
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001