MEDIUM ALIPHATIC SOLVENT NAPHTHA (PETROLEUM) ICSC: 1381
Machi 2001

White spirit type 0, regular flash point
Straight run kerosine
Straight run white spirit
CAS # 64742-88-7
RTECS #
UN # 1268
EC # 649-405-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
mnyunyizo wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni,
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 38°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 38°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kusinzia. Kichefuchefu. Kikohozi. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kikohozi. Kuhara. Kuumwa koo. Kutapika. (zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha mivuke ya misombo ya kikaboni yenye viwango mchemko vidogo).
Ainisho ya EU
Ishara: Xn
R: 65
S: (2-)23-24-62
Angalia: H
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


MEDIUM ALIPHATIC SOLVENT NAPHTHA (PETROLEUM) ICSC: 1381
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki na mpira.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°Cwakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera kidogo macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa viwango vya juu wa mvuke wake huweza kusababisha kupoteza fahamu. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini, husababisha kuharibika kwa utendaji. Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 138-178°C
Kiwango myeyuko: -48 - -26°C
Uzito wiani: 0.75-0.82 g/cm^3
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.2-0.6
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.0
Kiwango cha kumweka: 38-60°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 229-260°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.6-6.5
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
This is a mixture of n- and iso-paraffins, aromatic hydrocarbons and naphthenes. The contents of benzene is less than 0.1 % by volume. Depending on the raw material and the production processes, the composition and physical properties of this solvent can vary considerably. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Dalili za kichomi kinachotokana na kemikali hazijitokezi mpaka masaa au masiku machache yapite. Pia shauriana na ICSC 0361 Stoddard Solvent.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001