SODIUM CHROMATE ICSC: 1370
Machi 2001

Disodium chromate (VI)
Chromic acid, disodium salt
Disodium chromium tetraoxide
CAS # 7775-11-3 Na2CrO4
RTECS # GB2955000 Masi ya molekuli: 162
UN # 3288
EC # 024-017-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine.
Usigusishe na dutu ziwakazo.
Moto unapotokea katika eneo: maji mengi.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mchomo.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ishara: T, N
R: 49-43-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: A, E
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64c
Kavu. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


SODIUM CHROMATE ICSC: 1370
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO KAMA RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Mmumunyo huu katika maji ni besi dhaifu. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (as Cr): 0.05 mg/m^3 A1 (ACGIH 2000). Ainisho ya MAK IIIA2 (2000)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini, kusababisha kuharibika kwa utendaji

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji na mafigo, husababisha vitobo vya tenganisho la pua na kuharibika kwa figo. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 762°C
Uzito wiani: 2.7 g/cm^3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 53
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu sodium chromate tetrahydrate (CAS No. 10034-82-9).
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001