DIQUAT DIBROMIDE ICSC: 1363
Oktoba 2001

1,1'-Ethylene-2,2'-bipyridyllium dibromide
6,7-Dihydrodipyridol[1,2-a:2',1-c]pyrazinedium dibromide
9,10-Dihydro-8a-10a-diazoniaphenanthrene dibromide
CAS # 85-00-7 C12H12N2Br2
RTECS # JM5690000 Masi ya molekuli: 344.1
UN # 2781
EC # 613-089-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kutokwa damu puani.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Vidonda mdomoni. Maumivu ya tumbo. Kuhara. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. or bentonite clay in water, or Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ishara: T+, N
R: 22-26-36/37/38-43-48/25-50/53
S: (1/2-)22-28-36/37/39-45-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT7-III
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


DIQUAT DIBROMIDE ICSC: 1363
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 335°C huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni na bromidi hidrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: Diquat, kiwango cha kunuswa 0.5 mg/m³ (ngozi) A4 (ACGIH 2001). TLV: Diquat, kiwango cha kunuswa 0.1 mg/m³ (ngozi) A4 (ACGIH 2001).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mafigo, ini, mfumo wa moyo na mishipa na njia ya utumbo kusababisha kuharibika kwa utendaji na vidonda vya tishu. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri macho kusababisha mtoto wa jicho.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo 335°C
Uzito wiani: 1.2 g/cm^3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 70
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo °C: <0.0001
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -4.60 ifikapo 20 °C
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Kuhusu taaluma ya sumu ni kama ile ya diquati dibromidi monohidrati (CAS 6385-62-2) na diquati (CAS 2764-72-9). Usichukue nguo za kazi nyumbani. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001