1,2,3-TRIMETHYLBENZENE ICSC: 1362
Machi 2001

Hemimellitene
CAS # 526-73-8 C9H12
RTECS # DC3300000 Masi ya molekuli: 120.2
UN # 1993
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu linalokinza alkoholi, povu, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 44°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 44°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kuchanganyikiwa. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutapika. Kusinzia. Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35 Msimbo wa NFPA : H 0; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na vioksidishaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


1,2,3-TRIMETHYLBENZENE ICSC: 1362
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA (isoma zilizochanganyika)): 25 ppm; (ACGIH 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 176°C
Kiwango myeyuko: -25°C
Uzito wiani: 0.89 g/cm^3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.005
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.18
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 44°C
Jotoridi la kujiwasha: 470°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-6.6
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.7
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Pia shauriana na ICSC 1155 Mesitylene, 1389 Trimethyl benzene (mixed isomers).
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001