BERYLLIUM CARBONATE ICSC: 1353
Aprili 2000

Beryllium basic carbonate
CAS # 66104-24-3 Be2CO3(OH)2 / Be2CO5H2
RTECS # Masi ya molekuli: 181.07
UN # 1566
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.


MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ishara: T+, N
R: 49-25-26-36/37/38-43-48/23-51/53
S: 53-45-61
Angalia: A, E
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64c
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


BERYLLIUM CARBONATE ICSC: 1353
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 200° C huzalisha oksidi beriliamu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama (TWA)): 0.002 mg/m^3 A1 (ACGIH 1999). Ainisho ya MAK 2 (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Erosoli hii inakera njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye vumbi kunaweza kusababisha kichomi ya kemikali (chemical pneumonitis). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu, husababisha ugonjwa sugu wa berili (kukohoa, kupoteza uzito, kutokuwa na nguvu). Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Kwa sababu ya kutokuwa na habari dhahiri kuhusu dutu hii habari zilizoko kwa kadi hii zilitolewa kwa analogia ya muambatano ya beriliamu nyingine. Dalili ya kichomi kufuatia kukuzwa kwa muda mfupi haionyeshi mpaka siki tatu baadaye. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001