| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 72°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 72°C, uingizaji hewa.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Katisha salio kwa uangalifu na chokaa ya soda. Kisha osha kwa maji mengi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ishara: C R: 34 S: (1/2-)26-36-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G20C
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 0;
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii ni asidi kali ya kati. Humenyuka pamoja na besi na vioksidishaji vikali. Hushambulia metali nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 164°C Kiwango myeyuko: -7.9°C Uzito wiani (maji = 1): 0.96 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 57 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3 |
Kiwango cha kumweka: 72°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 452°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-10 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.79 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||