1-BROMOPROPANE ICSC: 1332
Novemba 1998

n-Propyl bromide
Propyl bromide
CAS # 106-94-5 C3H7Br / CH3CH2CH2Br
RTECS # TX4110000 Masi ya molekuli: 123.0
UN # 2344
EC # 602-019-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Ainisho ya EU
Ishara: Xn
R: 10-20
S: (2-)9-24
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G30 Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


1-BROMOPROPANE ICSC: 1332
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile bromidi hidrojeni. Humenyuka pamoja na besi kali na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kupoteza fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 71.0°C
Kiwango myeyuko: -110°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.35
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.25 mbaya
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 18°C: 13.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.3
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.4
Jotoridi la kujiwasha: 490°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.1
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001