| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Mfumo funge na uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ishara: T+, N R: 49-25-26-36/37/38-43-48/23-51/53 S: 53-45-61 Angalia: A, E Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| EMERGENCY RESPONSE | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64b
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE AU PODA NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV (kama (TWA)): 0.002 mg/m^3 A1 (ACGIH 1999). Ainisho ya MAK 2 (1999) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye vumbi kunaweza kusababisha kichomi ya kemikali (chemical pneumonitis). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Mfiduo huweza kusababisha kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu, husababisha ugonjwa sugu wa berili (kukohoa, kupoteza uzito, kutokuwa na nguvu). Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 3900°C Kiwango myeyuko: 2530°C Uzito wiani: 3.0 g/cm^3 Umumunyifu katika maji, ifikapo 20°C: hakuna |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili ya kichomi kufuatia kukuzwa kwa muda mfupi haionyeshi mpaka siki tatu baadaye. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2001 | |||