ALUMINIUM FLUORIDE (ANHYDROUS) ICSC: 1324
Oktoba 1999

Aluminium trifluoride
CAS # 7784-18-1 AlF3
RTECS # BD0725000 Masi ya molekuli: 84.0
UN # 1759
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80G18
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


ALUMINIUM FLUORIDE (ANHYDROUS) ICSC: 1324
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE CHA RISHAI, NYEUPE AU ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu ya florini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama F): 2.5 ppm; (as TWA) (ACGIH 1999) TLV (kama Al): 2 ppm; (ACGIH 1999) fluorides as F: 2.5 mg/m^3EC OELs
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Erosoli hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri mifupa, mfumo wa neva, husababisha mabadiliko ya mifupa kwa sababu ya florini (fluorosis), na kuharibika kwa mfumo wa neva.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango usablimishaji: 1272°C
Uzito wiani: 2.9 g/cm^3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.5
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 1238°C: 133
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
CAS 15098-87-0 and 32287-65-3 are for hydrated forms. Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001