CHROMOUS CHLORIDE ICSC: 1317
Aprili 2000

Chromium(II) chloride
Chromium dichloride
CAS # 10049-05-5 CrCl2
RTECS # GB5250000 Masi ya molekuli: 122.9
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.
Usigusishe na maji.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.

Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vilivyofunikwa. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


CHROMOUS CHLORIDE ICSC: 1317
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI KINACHONYONYA MAJI SANA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka ikiwa na vioksidishaji. Dutu hii huweza kupunguza kiasi cha oksijeni katika hewa katika maeneo funge. Humenyuka pamoja na maji kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1300°C
Kiwango myeyuko: 824°C
Uzito wiani: 2.8 g/cm^3
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
DATA YA MAZINGIRA
Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001