NITRIC OXIDE ICSC: 1311
Novemba 1998

Nitrogen oxide
Mononitrogen monoxide
(silinda)
CAS # 10102-43-9 NO
RTECS # QX0525000 Masi ya molekuli: 30.01
UN # 1660
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine.


MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kusinzia. Mchomo. Kichefuchefu. Kizunguzungu. Kuchanganyikiwa. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Kukosa pumzi. Degedege. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi

Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 5.1 na 8

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 736 Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 0; OX
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


NITRIC OXIDE ICSC: 1311
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI ILIYOBANWA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Inapogusana na hewa hutoa dioksidi nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 25 ppm; 31 mg/m^3 (ACGIH 1995-1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -151.8°C
Kiwango myeyuko: -163.6°C
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 0°C: 7.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.04
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001