METHOXYCHLOR ICSC: 1306
Machi 1999

1,1-(2,2,2-Trichloroethylidene)bis(4-methoxybenzene)
1,1,1-Trichloro-2,2-bis(p-methoxyphenyl)ethane
Dimethoxy-DDT
CAS # 72-43-5 C16H15C13O2
RTECS # KJ3675000 Masi ya molekuli: 345.7
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Tazama Kumeza. Tazama Vidokezo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


METHOXYCHLOR ICSC: 1306
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI MANJANO ISIYOKOZA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni (ICSC 0163) Humenyuka pamoja na vioksidishaji. Hushambulia baadhi ya plastiki na mpira.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 mg/m^3 (ACGIH 1998). MAK: 15 mg/m^3; III (1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo, mfumo mkuu wa neva, endapo kiasi kikubwa kimemezwa. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 89°C
Uzito wiani: 1.4 g/cm^3
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke: ndogo sana
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.68-5.08
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye samaki. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Maralate, Marlate, Metox, Prentox, Methoxicide ni majina ya kibiashara. Pia shauriana na ICSC #0034 DDT.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001