IMAZALIL ICSC: 1303
Novemba 1998

Allyl 1-(2,4-dichlorophenyl)-2-imidazol-1-ylethyl ether
1-(2-(2,4-Dichlorophenyl)-2-(2-propenyloxy)ethyl)-1H-imidazole
Enilconazole
CAS # 35554-44-0 C14H14Cl2N2O
RTECS # NI4776000 Masi ya molekuli: 297.2
UN #
EC # 613-042-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi

Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ishara: Xn, N
R: 20/22-41-50/53
S: (2-)26-39-60-61
Ainisho ya UN

EMERGENCY RESPONSE UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2001

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA


IMAZALIL ICSC: 1303
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANJANO KWA UTURUNGI KAMA FUWELE (OILI ILIYO MANGO).

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana kwa kutonesha au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu oksidi za nitrojeni na kloridi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri inihusababisha kuharibika kwa utendaji na vidonda vya tishu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: (imekadiriwa) 319-347°C
Kiwango myeyuko: 50°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.14
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana
Kiwango cha kumweka: 192°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.56
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Bromazil, Deccozil, Fecundal, Florasan, Freshgard, Fungaflor, Fungazil, Imaverol, Impala, Magnate, Sanazil ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


LEGAL NOTICE Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2001