LINURON ICSC: 1300
Novemba 1998

3-(3,4-Dichlorophenyl)-1-methoxy-1-methylurea
Urea, N'-(3,4-dichlorophenyl)-N-methoxy-N-methyl-
Methoxydiuron
CAS # 330-55-2 C9H10Cl2N2O2
RTECS # YS9100000 Masi ya molekuli: 249.1
UN #
EC # 006-021-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-40-48/22-50/53
S: (2-)-36/37-60-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LINURON ICSC: 1300
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile kloridi hidrojeni na oksidi za nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka kwa kunyunyiza au kutawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha anemia.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 93-94°C
Umumunyifu katika maji: hakuna (< 0.1g/100ml)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 24°C: 0.002
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.2
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mwani na mimea ya majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Afalon, Garnitan, Linex, Linorox, Linurex, Lorex, Sarclex, Scarclex ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005