1,4-DIMETHOXYBENZENE ICSC: 1297
Machi 2001

Benzene, 1,4-dimetoxy-
Hydroquinone dimethyl ether
p-Methoxyanisole
CAS # 150-78-7 C8H10O2
RTECS # CZ6650000 Masi ya molekuli: 138.17
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto. Usigusishe na vinavyoweza kuwaka.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO


Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyozibika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,4-DIMETHOXYBENZENE ICSC: 1297
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MAGAMBA NYEUPE, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 212°C
Kiwango myeyuko: 58-60°C
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: < 0.01
Kiwango cha kumweka: 88°C
Jotoridi la kujiwasha: 438°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-5.6
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.04
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu, kwa hiyo unahitajika uangalifu mkubwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005