3-METHYL-2-BUTENAL ICSC: 1294
Novemba 1998

3,3-Dimethylacrolein
3-Methylcrotonaldehyde
CAS # 107-86-8 C5H8O
RTECS # Masi ya molekuli: 84.12
UN # 2924
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na nyuso za moto.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 37°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 37°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kusinzia.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Osha kioevu kilichomwagika kwa maji mengi. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35
Isodhurika kwa moto. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
3-METHYL-2-BUTENAL ICSC: 1294
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO CHENYE HARUFU KALI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera njia ya upumuaji na husababisha ulikaji kwa macho na ngozi. Mfiduo husababisha kupungua fahamu. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji kusababisha vidonda vya tishu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 136°C
Kiwango myeyuko: -20°C
Uzito wiani: 0.9 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 15°C: 11
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.75
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.014
Kiwango cha kumweka: 37°C
Jotoridi la kujiwasha: 145°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.53
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Prenal ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005