NEOPENTYL GLYCOL DIACRYLATE ICSC: 1286
Novemba 1998

Acrylic acid, 2,2-dimethyltrimethylene ester
2,2-Dimethyl-1,3-propanediyl diacrylate
Dimethylolpropane diacrylate
2-Propenoic acid, 2,2-dimethyl-1,3-propanediyl ester
CAS # 2223-82-7 C11H16O4 / CH2CHCOOCH2C(CH3)2CH2OCOCHCH2
RTECS # AS8925000 Masi ya molekuli: 212.3
UN #
EC # 607-112-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali.

Ainisho ya EU
Alama: T
R: 24-36/38-43
S: (1/2-)-28-39-45
Angalia: [D]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Baridi. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NEOPENTYL GLYCOL DIACRYLATE ICSC: 1286
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU

HATARI KWA MWILI:
Mvuke hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu au vizimio vya miali ya moto, kuziba kwa matundu hufuatia.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.13kPa: 96°C
Kiwango myeyuko: 6°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.0
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 7.3
Kiwango cha kumweka: 115°C c.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. SR 247, Viscoat 247 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005