METHYL 2-CYANOACRYLATE ICSC: 1272
Oktoba 2000

2-Propenoic acid, 2-cyano-, methyl ester
2-Cyanoacrylic acid methyl ester
Mecrylate
CAS # 137-05-3 C5H5NO2 / CH2=C(CN)COOCH3
RTECS # AS7000000 Masi ya molekuli: 111.1
UN #
EC # 607-235-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Povu, poda kavu, dioksidi kaboni. USITUMIE maji.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 79°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 79°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Fyonza kioevu katika mchanga au kifyonzi ajizi. Acha mangoke. Vaa kingao cha uso kinachofaa. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 36/37/38
S: (2-)-23-24/25-26
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana, Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL 2-CYANOACRYLATE ICSC: 1272
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kwa haraka hasa kwa kuathiriwa na unyevu. Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho/gesi yenye sumu na yakerayo kama vile oksidi za nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): 0.2 (ACGIH 2000).
MAK: 2 ppm; 8 mg/m³; (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye mafusho kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Hugandia mara moja katika tishu hai.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 66°C
Kiwango myeyuko: -40°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.1
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 24
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Kiwango cha kumweka: 79°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.03 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005