ETHYLENE GLYCOL DIMETHACRYLATE ICSC: 1270
Oktoba 1995

2-Propenoic acid, 2-methyl-, 1,2-ethanediyl ester
Ethylene dimethacrylate
Methacrylic acid, ethylene ester
CAS # 97-90-5 C10H14O4 / CH2=C(CH3)C(O)OCH2CH2OC(O)C(CH3)=CH2
RTECS # OZ4400000 Masi ya molekuli: 198.2
UN #
EC # 607-114-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Kutoka kucha.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 36/37
S: (2)
Angalia: [D]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE GLYCOL DIMETHACRYLATE ICSC: 1270
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke hauzuiliki na unaweza kutengeneza polima katika matundu, kuziba kwa matundu hufuatia.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi au kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 260°C
Kiwango myeyuko: -40°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.05
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 478
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 101°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.87
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Ageflex EGDM, Nourycryl M221, Sartomer SR 206 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005