FLOCOUMAFEN ICSC: 1267
Oktoba 1995

4-Hydroxy-3-(1,2,3,4-tetrahydro-3-(4-(4-trifluoromethylbenzyloxy)phenyl)-1-naphthyl)coumarin
4-Hydroxy-3-(1,2,3,4-tetrahydro-3-(4-((4-(trifluoromethyl)phenyl)methoxy)phenyl)- 1-naphthalenyl)-2H-1-benzopyran-2-one
CAS # 90035-08-8 C33H25F3O4
RTECS # DJ3100300 Masi ya molekuli: 542.6
UN # 3027
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI! (See Notes).
Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Tazama Kumeza.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kizunguzungu. Kusinzia. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia. Kutokwa na damu (tazama Vidokezo).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FLOCOUMAFEN ICSC: 1267
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO NYEUPE.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile floridi hidrojeni na monoksidi kaboni (ona ICSC 0283 na ICSC 0023).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kuganda kwa damu kusiyokamili. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: cis-isoma: 181-191°C; trans-isoma: 163-166°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.0001 (hakuna)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: sio na maana
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 18.7
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.7 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa viumbe hai vya majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Dalili za kutoka damu hazijitokezi mpaka masiku baadaye. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Storm na Stratagem ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005