FLUTOLANIL ICSC: 1265
Aprili 2004

alpha,alpha,alpha-Trifluoro-3'-isopropoxy-o-toluanilide
N-(3-(1-Methylethoxy)phenyl)-2-(trifluoromethyl)benzamide
CAS # 66332-96-5 C17H16F3NO2
RTECS # CV5581320 Masi ya molekuli: 323.3
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto).
Usiwashe moto.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FLUTOLANIL ICSC: 1265
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ZISIO NA RANGI HADI NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na floridi hidrojeni, oksidi za nitrojeni, monoksidi kaboni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka kwa kunyunyiza au kutawanywa hasa kama poda.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 100-107°C
Uzito wiani: 1.3 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.001 (hakuna)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.7
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii yamechunguzwa lakini hayajaonekana.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005