3-METHYLPENTANE ICSC: 1263
Machi 1995

Diethylmethylmethane
CAS # 96-14-0 C6H14 / CH3CH2CH(CH3)CH2CH3
RTECS # none Masi ya molekuli: 86.2
UN # 1208 (hexanes)
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G30
Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
3-METHYLPENTANE ICSC: 1263
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka violently pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama hexane isomers): 500 ppm; 1760 mg/m³ (ACGIH 199?)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 63.3°C
Kiwango myeyuko: -118°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.66
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 20.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.97
Kiwango cha kumweka: <-20°C
Jotoridi la kujiwasha: 278°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-7.0
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005