| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE NYEUPE HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yakerayo na yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni besi kali ya kati. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana kabla ya kuyeyuka Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 93 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -2.62 (imekadiriwa) | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Trilon A ni jina la kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||