1,1,2,2-TETRABROMOETHANE ICSC: 1235
Oktoba 2004

Acetylene tetrabromide
Tetrabromoacetylene
sym-Tetrabromoethane
CAS # 79-27-6 C2H2Br4 / Br2CHCHBr2
RTECS # KI8225000 Masi ya molekuli: 345.7
UN # 2504
EC # 602-016-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Maumivu ya tumbo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 26-36-52/53
S: (1/2-)-24-27-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-III
Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 1;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,1,2,2-TETRABROMOETHANE ICSC: 1235
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO, NZITO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na bromidi kabonili, bromidi hidrojeni. Humenyuka pamoja na besi kali na vioksidishaji vikali. Hushambulia baadhi ya metali kama vile alumi, magnesiamu nazinki, na baadhi ya plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini kusababisha kuharibika kwa utendaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 243.5°C
Kiwango myeyuko: 0°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.96
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 24°C: 5.32
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 11.9
Jotoridi la kujiwasha: 335°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.8
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Muthmann's liquid pia hutumika kama kisawe.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005