| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 32°C. Hatari ya moto na mlipuko (tazama Hatari za Kikemikali).
|
Mfumo funge wa zaidi ya 32°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Nervousness. Kupungua hamu ya kula (anorexia).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Mibabuko nzito ya ngozi. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: Vazi linalokinga kemikali.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 and 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G61b
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hupolimisha kwa ukali sana kwa athari ya moto au mlipuko. Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu ya sianidi na oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Kinachotenganishwa na asidi kali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri ngozi kusababisha delayed burns na inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 159-160°C Uzito wiani (maji = 1): 1.00 Umumunyifu katika maji: wastani Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 44.5°C: 1.33 |
Kiwango cha kumweka: 42°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.39 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||