SODIUM TETRABORATE ICSC: 1229
Oktoba 1995

Sodium biborate
Sodium pyroborate
Boron sodium oxide
Fused borax
CAS # 1330-43-4 Na2B4O7
RTECS # ED4588000 Masi ya molekuli: 201.3
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kutokwa damu puani.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM TETRABORATE ICSC: 1229
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA RISHAI, NYEUPE AU SAHANI KAMA KIOO, ISO HARUFU. HUGEUKA ISIYOPENYEKA NURU INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi sodiamu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1994-1995)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kwa kumeza na kupitia ngozi iliyochipuka.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, mafigo, njia ya utumbo kwa kumeza kwa kiwango cha juu au kwa ngozi iliyochipuka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 1575°C
Kiwango myeyuko: 741°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.367
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 2.56
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Rasorite 65 ni jina la kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005