| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: kwanza ondoa mvuke asidi kwa maji mengi, kisha vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vya plastiki kavu. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 23/24/25 S: (1/2-)-26-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-III Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 0; |
Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ZISIO NA RANGI AU PODA NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na floridi hidrojeni na amonia. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na klorini trifluoridi kusababisha athari ya mlipuko. Hushambulia kioo na metali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kama fluorini) 2.5 mg/m³ kama TWA; A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: (kama F) (sehemu ndogo ya kuvutwa mapafuni) 1 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(4); kunyonywa na ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2005). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mifupa na meno kusababisha mabadiliko ya mifupa na meno kwa sababu ya florini (fluorosis). | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: hujisablimisha Uzito wiani: 1.01 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 45.3 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||