THALLIUM CARBONATE ICSC: 1221
Machi 2002

Carbonic acid, dithallium(1+) salt
Dithallium carbonate
Thallous carbonate
CAS # 6533-73-9 Tl2CO3
RTECS # XG4000000 Masi ya molekuli: 468.78
UN # 1707
EC # 081-002-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Tazama Kumeza.
Mavazi ya kinga. Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuumwa kichwa. Udhaifu. Uchungu kwa miguu. Kutoona vizuri. Kupotea kwa nywele. Kutotulia. Degedege. Moyo kuenda haraka. Ona Vidokezo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu). Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+, N
R: 26/28-33-51/53
S: (1/2-)-13-28-45-61
Angalia: [A]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-II
Kilichofungwa vizuri. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
THALLIUM CARBONATE ICSC: 1221
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Tl na misombo mumunyifu): 0.1 mg/m³ kama TWA (ngozi) (ACGIH 2001)
Ainisho ya MAK: IIb, kama Tl na misombo mumunyifu (2001)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kumeza na kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa neva, mafigo na mfumo wa moyo na mishipa. Yaweza kusababisha kupotea kwa nywele na kudhoufika kwa makucha. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva na yaweza kusababisha kupotea kwa nywele. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 272°C
Uzito wiani: 7.1 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 5.2
DATA YA MAZINGIRA
Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa mfano kufuata mwishono wa vyakula kwa mboga na viumbe vya majini. Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege na mamalia. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Dalili ya madhara ya thaliamu kwa kawaida hutokea polepole; dalili kwa tumbo (kusikia kama kutapika, kutapika, uchungu kwa tumbo) hutokea kwa kawaida baada ya saa chache baada ya mfiduo, na kuhusu neva dalili zingine yaweza kutokea baada ya siku 2-5. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Ona ICSC 0077 (Thallium), 0336 (Thallium sulfate).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005