SODIUM ARSENATE DIBASIC ICSC: 1208
Machi 1999

Arsenic acid disodium salt
Disodium arsenate
Disodium hydrogen arsenate
CAS # 7778-43-0 AsHNa2O4 / HNa2AsO4
RTECS # CG0875000 Masi ya molekuli: 185.9
UN # 1685
EC # 033-005-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Udhaifu. (Tazama Kumeza).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kuhara. Maumivu ya tumbo. Kuhisi hali ya kuungua kifuani na mdomoni. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-23/25-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [A, E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64b
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM ARSENATE DIBASIC ICSC: 1208
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU FUWELE ISO RANGI HADI NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka pamoja na asidi kutoa gesi yenye sumu ya arsini (ICSC # 0222). Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji kama vile chuma, alumi na zinki, ikitoa mafusho yenye sumu ya arseniki na arsini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama As): 0.01 mg/m³ A1 (ACGIH 1998)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa moyo na mishipa, mfumo mkuu wa neva, mafigo, kusababisha uvimbe wa tumbo na chango (severe gastroenteritis), upungufu wa maji na elektroliti mwilini, ugonjwa wa moyo, kuharibika kwa figo, mshtuko na kifo. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva wa pembeni, ngozi, kiwamboute, uboho, mafigo na ini, kusababisha uvimbe wa neva (neuropathi), kugeuka kwa rangi ya asili vitobo vya tenganisho la pua, vidonda vya seli za damu, kuharibika kwa ini na ini kuwa ngumu (cirrhosis). Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii inaweza kusababisha ulemavu kwa watoto wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 57°C
Uzito wiani: 1.87 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 15°C: 61
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji ya ardhini, maji na viumbe viishivyo ardhini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005