| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na dutu ziwakazo na maunzi yasiokubaliana.
|
Maji mengi.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga.
|
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Kichefuchefu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51G02
|
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni na oksidi ya zinki. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na kaboni, shaba, salfidi za metali, fosforasi na sulfuri. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko: takribani 110°C Uzito wiani (maji = 1): 2.07 (heksahidrati) Umumunyifu katika maji: vizuri |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa wanyama na wadudu wenye magamba.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutia maji huongeza kiwango cha dhara. Viwango myeyuko vinginevyo: 45.5°C (trihidrati); 36.4°C (heksahidrati). Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||