NITROGEN (LIQUIFIED) ICSC: 1199
Machi 1999

Liquid nitrogen
Nitrogen (refrigerated liquid)
Nitrogen (cryogenic liquid)
(kilichooevuka)
CAS # 7727-37-9 N2
RTECS # QW9700000 Masi ya molekuli: 28.01
UN # 1977
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi Ukosefu na hewa. Tazama Vidokezo.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Zaidi tazama Ngozi.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Silinda maalum isiyopitisha joto.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 112 / 20G48
Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0;
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITROGEN (LIQUIFIED) ICSC: 1199
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KISICHO HARUFU, BARIDI MNO

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa, endapo baridi, na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
Asfiksianti sahili (ACGIH 1998)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -196°C
Kiwango myeyuko: -210°C
Uzito wiani: 0.808 kg/l ifikapo kiwango mchemko ya kioevu
Umumunyifu katika maji: mbaya
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005