CALCIUM ICSC: 1192
Oktoba 1994

Elemental Calcium
CAS # 7440-70-2 Ca
RTECS # EV8040000 Masi ya atomi: 40.1
UN # 1401; 1855 (kalsiamu paroforiki)
EC # 020-001-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu. Inashika moto haraka ikiwa imeshakwa nyororo. Hutoa gesi inayoshika moto ikigusa maji au hewa yenye unyevu. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na maji na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine. USITUMIE maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na maji na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali.

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: F
R: 15
S: (2-)-8-24/25-43
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3; 4.2 (kalsiamu pairoforiki)
Kikundi Ufungashaji cha UN: II; I (kalsiamu pairoforiki)
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43G12; 42G13 (pairoforiki)
Msimbo wa NFPA: H 1; F 1; R 2; W;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana. Tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Weka katika gesi ajizi. Weka chini ya mafuta ghafi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CALCIUM ICSC: 1192
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FEDHA INAYONG'ARA (KAMA IMEKATWA HAPO); HUGEUKA KUWA KIJIVU IKIGUSWA NA HEWA YENYE UNYEVU.

HATARI KWA MWILI:
Inashika moto haraka ikiwa imeshakwa nyororo.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na maji, asidi imezimuliwa na alkoholi na kutoa gesi hidrojeni inayoweza kuwaka haraka. Humenyuka pamoja na halojeni. Huwaka kwa hewa. Huweza kupasuka ikiguswa na alkali hidroksidi au kabonati.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1440°C
Kiwango myeyuko: 850°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.54
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji, povu, haloni na dioksidi kaboni. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005