ALUMINIUM SULFATE ICSC: 1191
Oktoba 1994

Aluminium sulphate
Aluminium trisulfate
Alum
CAS # 10043-01-3 Al2S3O12 / Al2(SO4)3
RTECS # BD1700000 Masi ya molekuli: 342.14
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Inababua. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na besi kali. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ALUMINIUM SULFATE ICSC: 1191
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU FUWELE NYEUPE, ING'ARAYO, ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile oksidi za sulfuri. Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati. Humenyuka pamoja na alkali na Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama chumvi mumunyifu ya Al): 2 mg/m³ (ACGIH 1993-1994)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 770°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.71
Umumunyifu katika maji: vizuri
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa samaki.
VIDOKEZO
Cake alum, pickle alum, filter alum, papermaker's alum na pearl alum ni majina mengi na ya kawaida ya sulfati alumini. Hutokea kiasili kama madini ya alunogenite.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005