METHYL SILICATE ICSC: 1188
Oktoba 1997

Tetramethyl silicate
Tetramethyl orthosilicate
Tetramethoxy silane
CAS # 681-84-5 C4H12O4Si / (CH3O)4Si
RTECS # VV9800000 Masi ya molekuli: 152.3
UN # 2606
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 20°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 20°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.

MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Upofu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G60
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL SILICATE ICSC: 1188
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm; 6 mg/m³ (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzivapour kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 121°C
Kiwango myeyuko: -2°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.02
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.3
Kiwango cha kumweka: 20°C c.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Viwango myeyuko vinginevyo: -8°C. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005