n-HEPTANOIC ACID ICSC: 1179
Oktoba 1994

Enanthic acid
n-Heptylic acid
n-Heptoic acid
CAS # 111-14-8 CH3(CH2)5COOH / C7H14O2
RTECS # MJ1575000 Masi ya molekuli: 130.2
UN # 3265
EC # 607-196-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 34
S: (1/2-)-26-28-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na besi, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
n-HEPTANOIC ACID ICSC: 1179
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU ANGAVU KAMA MAFUTA

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 223°C
Kiwango myeyuko: -7.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: mbaya (0.24 g/100 ml)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 78°C: 133.3
Kiwango cha kumweka: >110°C c.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005