| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Inababua. Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Mchomo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vikavu vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G61a
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO ISIYOKOZA, KIFUKACHO HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na kloridi hidrojeni na oksidi za sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na besi kama vile amonia na dutu nyingine nyingi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na maji na mvuke kutoa mafusho yenye sumu na babuzi (kloridi hidrojeni). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi au kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Inayotoza machozi. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 97.3kPa: 161°C Kiwango myeyuko: -32°C Uzito wiani (maji = 1): 1.5 Umumunyifu katika maji: mmenyuko Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.27 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01 Kiwango cha kumweka: >110°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||