T.E.P.P. ICSC: 1158
Aprili 1994

Tetraethyl pyrophosphate
Diphosphoric acid, tetraethyl ester
Tetraethyl diphosphate
CAS # 107-49-3 C8H20O7P2 / (C2H5O)2-PO-O-PO-(OC2H5)2
RTECS # UX6825000 Masi ya molekuli: 290.2
UN # 3018
EC # 015-025-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kichefuchefu. Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kizunguzungu. Upotevu wa mtingiko - kupatana. Degedege. Kutapika. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Mibabuko ya ngozi. Maumivu. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Msongo/mfinyo wa jicho. Kiwaa. Kuumwa kichwa.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Usimtapishe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 27/28
S: (1/2-)-36/37/39-38-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G44
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
T.E.P.P. ICSC: 1158
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI KISICHO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha zaidi ya 150°C gesi inayoweza kuwaka (ethilini) na mafusho yenye sumu kama vile oksidi za fosforasi. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako. Husababisha kulika kwa metali za kawaida.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.004 ppm; 0.047 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1991-1992)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi, kwa kumeza na kupitia kwa macho.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C, wakati wa kunyunyiza kwa kasi zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha degedege, kutoweza kupumua na kifo. Kizuizi cha kolinesterasi. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 170°C
Kiwango myeyuko: tazama Vidokezo
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: vizuri
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 10
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: tazama Vidokezo
Jotoridi la kujiwasha: tazama Vidokezo
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.94
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa mamalia, ndege, nyuki na viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Wakati wa kuyeyuka, huganda na kuwa kama kioo kwa 0°C. Kiwango cha kumweka haijulikani. Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Bladan, Fosnex, Gy-Tet 40, HETP, Hexaethyltetraphosphate, Killex, Kilmite, Lethalaire, Licophosphate, Nifos T, Pyfos, Pyro-Phos, Teep, Tetradusto 100, Tetron, Tetraspa na Vapotone ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005